Header ads

Header ads
» » UTAFITI:: Watu wengi wanaopenda kutia picha za paka katika mitandao ya kijamii hawana wapenzi



IDADI kubwa ya watu wanaopenda kutia picha za paka katika mitandao ya kijamii hawana wapenzi, utafiti umebaini.
Watafiti wa mtandao wa Facebook pia walibaini kuwa watu wanaopenda kutia picha za mbwa mitandaoni wameolewa, wameoa au wana wapenzi.


Romania International Cat Show Watafiti walichunguza akaunti za Facebook za watu 160,000 nchini Amerika na wakabaini kuwa asilimia 30 ya watu wanaotia picha za paka mitandaoni hawana wapenzi.
Utafiti huo unaonyesha kuwa walio na mazoea ya kuweka mitandaoni picha za mbwa wanapenda kutangamana na watu wengine ilhali wanaopendelea picha za paka wakifurahia maisha ya upweke.
Heather Marcoux
Utafiti huo wa Facebook uliochapishwa katika tovuti: www.research.facebook.com unaonyesha kuwa tabia za watu wanaofuga paka au mbwa hufanana kwa kiasi fulani na wanyama hao.
“Watu wanaotia mitandaoni picha za paka hupendelea kuandika maneno kama vile ‘nimechoka’ ilhali wanaotia picha za mbwa wakiandika ‘nimefurahi’,” ukasema utafiti huo.


Chanzo> www.cbc.ca

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post