Header ads

Header ads
» » Kutana na Wazee Waliofunga Ndoa wakiwa na Umri mkubwa zaidi

 

George Kirby akiwa na mke wake Doreen Lucky
George Kirby akiwa na mke wake Doreen Lucky
George Kirby mwenye umri wa miaka 103 na Doreen Lucky mwenye umri wa miaka 91 watafunga pingu za maisha mwezi Juni tarehe 13 mwaka huu.
Kwa mujibu wa gazeti la Uingereza la Daily Mail, wapenzi hao walikutana mwaka 1988 na tangu mwaka huo walikuwa hawajaamua kufunga ndoa.
Bwana harusi George alimposa mpenzi wake Doreen katika siku ya wapendanao.
George alipohojiwa kwa nini waliamua kuoana baada ya miaka yote hii alijibu kuwa, “nadhani hata kama ningekuwa sijashtukia umri wangu, sasa ndio wakati mwafaka wetu wa kufunga ndoa maana Doreen hunifanya nijihisi kijana.”
Wanandoa hao waliongeza kuwa, “Hatukuchukuwa uamuzi wa kufunga ndoa kwa ajili ya kuvunja rekodi yoyote ya dunia, bali kwa sababu tunapendana na tumeona kwamba kufunga ndoa kwa wakati huu ndio hatua bora kwenye maisha yetu.”

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post