Header ads

Header ads
» »Unlabelled » Je MBOWE Kwenda UBUNGO kuwashawishi madereva kusitisha mgomo, alikuwa akitafuta umaarufu wa kisiasa?!! .


Kitendo cha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwenda katika Kituo cha Mabasi cha Ubungo (UBT) kuwashawishi madereva kusitisha mgomo kimepokewa kwa hisia tofauti na wananchi.
Wakizungumza jana, baadhi ya wananchi walisifu kitendo hicho huku wengine wakisema alikuwa akitafuta umaarufu wa kisiasa.
Hata hivyo, Mbowe aliwaambia waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Chadema kuwa aliamua kwenda kuzungumza na madereva hao kwa nia ya kuwaeleza kuwa mgomo wao unazidi kuwatesa wananchi na kwa kuwa ujumbe wao ulishafika.
Alisema Serikali imeshindwa kutatua matatizo ya wananchi na hivyo migomo inahitajika ili kuisukuma Serikali kutatua matatizo ya wananchi.
“Mgomo huo ni matokeo ya Serikali kupuuza madai yao kwa muda mrefu na kauli aliyoitoa (mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul) Makonda inaonyesha ni aina gani ya viongozi tuliona nao hapa nchini. Wamekosa majibu ya kumaliza tatizo hilo,” alisema.
Mbowe alisema hata kitendo cha Makonda kuahidi kushughulikia matatizo ya madereva ifikapo leo na yasipotatuliwa ataungana nao, ni hatari.
“Haya ni matokeo ya kuwa na viongozi wasio na sifa,” alisema Mbowe.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wamechukulia kitendo cha mwenyekiti huyo wa Chadema kuwa ni cha kujitafutia umaarufu kirahisi.
Mhadhiri mwandamizi ambaye ni Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Emmanuel Mallya alisema katika mazingira kama hayo siyo jambo la ajabu kuona mwanasiasa akijitokeza.
“Mwanasiasa yeyote anapoona migogoro kama hiyo, ni rahisi zaidi kuitumia nafasi hiyo ili kujijengea mazingira mazuri ya kukubalika kisiasa, iwe kwa nia nzuri au vinginevyo kutokana na udhaifu uliojitokeza,” alisema Mallya.
Mallya alisema mgomo huo haukutakiwa kuchanganywa na itikadi za kisiasa kutokana na unyeti wake.
“Siyo jambo la kupendekeza kwa chama chochote cha kisiasa kutaka kugeuza mgomo huo kuwa ajenda ili kujinufaisha kisiasa,” alisema.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post