Header ads

Header ads
» » Aliyerusha Risasi Hewani katika Ofisi za Chadema Ahukumiwa Kwenda Jela Miez 6 Au Kulipa Faini sh.2000


Kada wa CCM Ahmed Ismail aliyerusha risasi hewani katika ofisi za Chadema wilayani Bariadi amehukumiwa kwenda jela miezi sita au kulipa faini Sh2,000 baada ya kukutwa na hatia.
 
Ismail alikuwa akikabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya silaha.
 
Mwendesha Mashtaka, Yamiko Mlekano alidai mahakamani hapo kuwa Aprili 22, mwaka huu, saa 10 jioni mshtakiwa huyo alikwenda kwenye mkutano wa hadhara wa CCM katika Mtaa wa Isanga akiwa na bastola.
 
Alidai kuwa siku hiyohiyo, akiwa kwenye msafara wa Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge alitoa silaha hiyo hadharani kisha kufyatua risasi tatu karibu  na ofisi za Chadema wilayani humo kinyume cha sheria.
 
Mshtakiwa alipotakiwa kujitetea kabla ya hukumu, aliomba Mahakama imuonee huruma kwa kuwa hakujua kama ilikuwa ni makosa.
 
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Aidon Mwilapwa alitoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi. Mshtakiwa huyo aliachiwa huru baada ya kulipa faini.
 
Siku ya tukio Ismail alizua taharuki baada ya kufyatua risasi tatu wakati msafara wa Chenge ulipokutana na ule wa Chadema mjini Bariadi, Simiyu.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post