Header ads

Header ads
» » Vurugu zasababisha kikao cha bunge kuahirishwa

Bunge limehairishwa hadi jioni baada ya vurugu kuibuka kwa baadhi ya Wabunge wakitaka hoja ya kuhairisha mchakato wa kura ya maoni ujadiliwe maana na kura ya maoni isogezwe mbele maana muda hautoshi na wananchi wamejitokeza kwa wingi kujiandikisha.
Mnyika alisimama na kutoa hoja
Mnyika: "Nimesimama kupata idhini kwa mujibu wa kanuni ili shughuli za bunge zisitishwe badala yake tujadili zoezi la uandikishaji nchi nzima, mpaka sasa zoezi halijakamilika hata kwa mkoa mmoja tu wa Njombe, jambo hili ni la dharura na ilishatolewa na ukaagiza kamati ishughulikie, majibu tupate kikao hiki na leo tunafunga mkutano hamna kitu"
Makinda: Hoja hii inafanana na ile ya kwanza, nimesema majibu mtajibiwa baadaye
Wabunge walisimama na kupiga kelele wakitaka majibu ndipo Spika Anna Makinda akalazimika kusitisha Bunge hadi jioni.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post