Header ads

Header ads
» » Kufuatia Mashambulizi ya Wazawa dhidi ya Wageni Nchini Afrika Kusini, Watnzania 26 Wamerejea Nyumbani.


Kundi la Watanzania 26 limerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini leo tarehe 25 Aprili, 2015 kufuatia mashambulizi ya wazawa dhidi ya wageni. Kundi hilo la kwanza kurejea nyumbani liliwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa 11 alfajiri na Ndege ya Fast Jet.
Watanzania hao walikuwa wanaishi katika kambi za 


dharura za Isipingo na Phoenix zilizopo jijini Durban. Walisindikizwa kurudi nyumbani na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Bw. Elibahati Lowassa. Zoezi la kuwarejesha wananchi hao lilisimamiwa na kuratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.
Wakati huo huo, Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umepata taarifa kuwa kuna Watanzania wengine wapatao 20 wanaishi kwenye Kambi ya Hillbrough jijini Johannesburg. Ubalozi umetuma Afisa kwenda katika kambi hiyo ili kufanya uhakiki wa taarifa hizo kwa madhumuni ya kuwarejesha nyumbani Tanzania haraka iwezekanavyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
25 Aprili 2015 

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post