Header ads

Header ads
» » Dr. Slaa: CHADEMA Tukiingia Ikulu Tutaifuta Katiba Inayopendekezwa na Kuanza Mchakato Upya



 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa (pichani), amesema kuwa iwapo Watanzania watakipa ridhaa chama hicho ili kushika dola katika uchaguzi wa mwaka huu, kitu cha kwanza watakachoanza nacho ni kuifuta Katiba inayopendekezwa sasa na kuanzisha mchakato wa Katiba yenye maslahi ya wananchi.

Dk. Slaa alisema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapa katika viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro na kuudhuriwa na umati mkubwa wa watu.

Alisema Katiba iliyopendekezwa na kupigiwa debe hivi sasa na Chama cha Mapinduzi(CCM) haina maslahi yoyote kwa wananchi wa pande zote mbili za Muungano na kwamba ipo kwa ajili ya kunufaisha viongozi wachache, hivyo wakiingia madarakani wataifuta mara moja.

Dk. Slaa alisema kuwa Katiba ya Wananchi wa pande zote mbili ambayo inagusa maslahi yao na kutetea haki zao ni rasimu iliyopelekwa katika Bunge Maalum iliyoandaliwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.




“Sote tunamfahamu Jaji Warioba, alikuwa Waziri Mkuu wa nchi na ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba na katika tume yake alikusanya mapendekezo yenu nyinyi wananchi, lakini kwa maslahi yao hasa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakatoa maoni yenu na kuweka maslahi yao ,sasa nyie tuchagueni tuingie Ikulu tuwarudishie Katiba yenu,” alisema Dk. Slaa.

Alisema Jaji Warioba ni mmoja wa viongozi wachache wenye uchungu na nchi hii na ndio maana wakati wa kukusanya maoni alizingatia maslahi ya wananchi wote bila kuangalia rangi, kabila pamoja na itikadi ya vyama vya siasa.

Dk. Slaa alisema kuwa katika mchakato watakaounzisha endapo watapewa dola na Watanzania ni kuunganisha mapendekezo yote ya wananchi waliyotoa katika iliyokuwa tume ya Jaji Warioba ukiwamo muundo wa Serikali tatu ambao unakatiliwa na Serikali ya CCM.

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post