Header ads

Header ads
» » KUTANA NA MTU ALIYENUSURIKI KIFO BAADA YA KUCHOMWA NA CHUMA SENTIMITA 20 KICHWANI


Liu Fenghe akiwa hospitali na chuma kichwani.
Picha ya X-ray ikionyesha jinsi chuma hicho kilivyoingia kichwani mwa bwana Liu. (Picha: HAP/Quirky China News/Rex)
FUNDI majengo Liu Fenghe wa nchini China, amenusurika kifo baada ya kuchomwa na chuma kichwani na kuzama inchi 8 ambazo ni sawa na sentimita 20.
Liu alikuwa akiongea na rafiki yake na kwa bahati mbaya alidondokewa na chuma hicho kilichomchoma kichwani.
Rafiki yake Liu aitwaye Zhang anasema: "Ilikuwa ghafla. Kabla sijafanya chochote Liu alikuwa katika dimbwi la damu."
Inadhaniwa kuwa chuma hicho kilidondoka kutoka ghorofa ya 25 ya jengo walilokuwemo mafundi hao mpaka kusababisha maafa hayo.
Madaktari walimfanyia upasuaji wa haraka katika hospitali iliyopo jimbo la Shanghe nchini China na kueleza kuwa Liu hayupo tena katika hatari japo bado haijajulikana ni lini ataweza kurudi kazini.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post