Header ads

Header ads
» » Maboresho yazidi kuongezeka kwenye programu ya WhatsApp, Utaweza ku-like post kama Facebook vile

Kitufe cha ‘‘Like’’ katika WhatsApp

Programu ya mawasiliano ya WhatsApp inaelekea kufuata nyao za Facebook kwa kuiga baadhi ya maboresho.
Katika harakati za kuboresha huduma zake, WhatsApp inadaiwa kujiandaa kuweka kitufe cha ‘‘Like’’ kama ilivyokuwa kwenye mtandao wa jamii wa Facebook.
Kulingana na tetesi zilizotolewa, kitufe hicho cha ‘‘Like’’ kitaweza kutumiwa wakati mtu atakapopokea ujumbe ambao hawezi kuujibu kwa muda ule.
Hivyo basi, mtumiaji ataweza kujibu kutumia kitufe cha ‘‘Like’’ ili kudhihirisha kuwa ameupokea kama ilivyokuwa katika matumizi ya alama za rangi ya buluu zinazoashiria kusomwa kwa ujumbe uliotumwa.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post