Header ads

Header ads
» » KESI YA MUME WA FLORAH MBASHA YASOGEZWA MBELE


Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam jana ilitumia nusu sasa tu kusogeza mbele kesi inayomhusu Emmanuel Mbasha, huku pia ikishindwa kumsomea maelezo ya awali kutokana na wakili wake kuwa safarini.

Kesi hiyo sasa itatajwa tena Julai 23 mwaka huu. Hatua hiyo ni baada ya mahakama kuelezwa na mwakilishi wa wakili wa mshtakiwa, Daudi Malima kuwa wakili wa Mbasha, Mathew Kakamba yupo safarini Arusha.

Mbasha, mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili nchini, Flora, anakabiliwa na mashtaka mawili ya ubakaji.

Mbali na kuahirishwa kesi hiyo, mahakama hiyo pia ilimtaka wakili wa mshtakiwa kutoa ufafanuzi kutokana na kutofautiana taarifa zilizowasilishwa mahakamani kati ya mshtakiwa na wakili wake.
Mwendesha mashtaka na wakili wa Serikali, Gloria Mwenda alisema shauri hilo lilikuja ili kusomewa maelezo ya awali.

Baada ya Hakimu Wilbarforce Luhwago kutoa ruhusa ya usomwaji kuendelea, mshtakiwa alinyoosha mkono na kueleza kuwa wakili wake alikuwa njiani kuja mahakamani hapo, jambo ambalo mahakama ilikubali na kuongeza nusu saa ili kusubiri.

Kesi ilipoitwa mara ya pili saa 3:00 asubuhi, wakili aliyejitambulisha kama David Malima, aliieleza mahakama kuwa alikuwa amepokea maelekezo ya kumsaidia wakili wa mshtakiwa, Mathew Kakamba ambaye amesafiri kwenda Arusha.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post