Header ads

Header ads
» » TETESI: ARSENAL INAMBANGO WA KUMPA THIERY HENRY UKUFUNZI WA TIME HIYO

Steve Bould na kocha wa Arsenal Arsene Wenger
Arsenal ina mpango wa kumpatia aliyekuwa mshambulizi wa timu hiyo Thiery Henry fursa ya ukufunzi katika timu hiyo kulingana na gazeti la daily mail.
Kandarasi ya raia huyo wa Ufaransa katika kilabu ya New York Red Bulls inatarajiwa kuisha mwisho wa msimu wa ligi ya soka ya marekani MLS mwezi ujao na hajasema ni hatua gani anayotarajia kuchukua.
Wengi wanaamini kwamba kampeni hiyo itakamilisha harakati zake kama mchezaji na huenda Arsene Wenger akamchukua katika kilabu hiyo.
Na alipoulizwa iwapo Henry anaweza kurudi katika kilabu hiyo kama kocha ,Wenger alijibu kwamba hakuna lisilowezekana.''Mimi huwakaribisha watu ambao wameichezea timu hii''.
''Hatahivyo ni lazima ajifunze kazi hii mwanzo'',.
Nimewaona wengi ambao wana uwezo lakini wameshindwa katika fursa yao ya kwanza kwa kuwa hawakuwa tayari.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post