WADADA WAKIUMANA KWA HASIRA |
Exclusive, breakiiing nyeusiiiiiii......blog yako ya bAHTSMA yaliyopitiliza imefanya utafiti wa hali ya juu kuhusu picha ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii na isiyo ya kijamii dunia nzima kama vile cnnblogspot,bibisi na kadhalika, ikiwa na maelezo ambayo mtandao huu unayapinga kwa nguvu zote za giza. Utafiti uliofanywa na blog hii kwa kushirikisha mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu na yale ya hakimiliki imegundua kuwa watu wengi wanachokiona hapa sicho kilicho au tuseme kilicho sicho kilivyo, au tuseme kilivyo sicho ndicho, ushanijua ee. Kwa kutumia utaalamu wa hali ya juu sana ambao utaalamu huu ulitumika katika kufanya utafiti wa kugundua kama Saddam Hussein ana mabomu ya nyuklia mfukoni au la, na utaalamu huu ulitumika pia katika kutafuta gesi Ntwara, mtandao huu na washirika wake wamegundua mambo kadhaa yaliyokuwa yakitokea wakati wa kupigwa kwa hii picha. Kwa kupitisha kwenye International Chinese Analogue Digital Scanner(ICADS), imeonekana picha hii ni feki, lakini baada ya kuiscan kwenye Mobile Colour Text Scanner(MCTS) ikaonekana kuwa kulikuwa na kelele za watu wengi wakati picha hii inapigwa, na pia kulikuwa na harufu za pafyum mchanganyiko na udi wa Zanzibar. Hii ilisaidia kucreate atmosphere ambayo ilileta mitandao mingi kuona kile ambacho kiukweli kilikuwepo hakipo. Utafiti huu umegundua kuwa picha hii inaashiria kulikuwa na ugomvi mkali kati ya wanaonekana katika picha maana hapa walifikia hatua ya kutaka kuumana kwa hasira kali iliyokuwa imewazidi, lakini kumbe mmoja alikuwa katoka kula mishkaki yenye pilipili iliyowafanya wote wafunge macho kwa uchungu wa pilipili hiyo. Uchunguzi pia umegundua kuwa katikati ya hawa wadada kuna mdada mwingine aliyekuwa nyuma yao, ambaye ni wazi anatumia mkorogo wa hali ya juu, kwani vidole vyake tu vilivyoshika glasi ya ulanzi vinaonekana vikiwa vimeathirika na mkorogo. Mtandao huu unaendelea na upelelezi kujua je ugomvi huu uliishia wapi? na je, kuna mtu labda alinyofolewa midomo au ulimi?. Fuatilia mkasa mzima kwenye blog hii yenye watafiti waliobobea ambao kauli mbiu yetu ni..... unaweza kukwepa mvua lakini sio utafiti wetu.
Mkurugenzi Mwenye Enzi
Mkurugenzi Mwenye Enzi